Mabadiliko katika mfumo wa utangazaji kutoka mfumo wa analojia kwenda katika mfumo wa dijitali ni utaratibu ambao unaendelea ulimwenguni kote. Mabadiliko haya yanatokana na makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya masuala ya mawasiliano yaani International Telecommucations Union yaliyofanyika mwaka 2005 huko Geneva, Uswisi. Makubaliano ya nchi wanachama ni kuzima kabisa matangazo katika mfumo wa analojia na kutumia mfumo wa utangazaji wa dijitali ifikapo tarehe 17 Juni 2015.
Ili
kuhakikisha mabadiliko haya yanafanyika kwa ufanisi, tija na pia kutoa muda wa
kutosha wa kutekeleza mabadiliko haya, mwaka 2005 Serikali ilianza mchakato wa
uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali ambao ulihusisha
wadau wote, wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari na vituo vya utangazaji wa
televisheni, hatua kwa hatua, hadi kuridhia ratiba nzima ya uzimaji wa mitambo
ya analojia. Kwa kifupi mchakato wa uhamaji ulipitia hatua zifuatazo:
Mwaka 2005: Waraka
wa kwanza wa mashauriano (consultative document) kuhusu umuhimu na faida za
kuhama kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali ulitayarishwa na
kusambazwa kwa wadau wote;
Mwaka 2006: Waraka
wa pili wa mashauriano na mapendekezo ya muundo wa leseni kwenye mfumo wa
utangazaji wa teknolojia ya dijitali ulitayarishwa na kusambazwa kwa wadau
wote;
Mwaka 2007: Kamati
ya kiufundi inayoshughulikia uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia
kwenda dijitali iliundwa;
Mwaka 2007: Mkutano
mkuu uliojumuisha vituo vyote vya utangazaji nchini ulifanyika Bagamoyo
kupitisha maazimio ya mfumo wa leseni za utangazaji utakaotumika kwenye mfumo
wa dijitali;
Mwaka 2010: Kampuni
tatu (3) zilipewa leseni za ujenzi wa miundombinu ya utangazaji ya dijitali.
Kampuni tatu zilizopewa leseni za kusambaza matangazo ya dijitali ni Agape
Associates Limited, Basic Transmission Limited, na Star Media (T) Limited.
Kampuni hizo zilipewa leseni baada ya kuthibitisha kuwa zina uwezo wa kujenga
miundombinu ya kurushia matangazo katika mfumo wa dijitali;
Mwaka 2010: Kamati
ya Kitaifa ya Kuratibu Mabadiliko ya Utangazaji toka mfumo wa analojia kwenda
dijitali iliundwa. Kamati hii hukutana kila baada ya miezi mitatu kutathmini
maendeleo ya ubadilishaji wa mfumo wa utangazaji;
Mwaka 2011: Kampeni
ya Kitaifa ya kuelimisha umma kuhusu mabadiliko ya mfumo wa utangazaji
ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ili
kuhakikisha kuwa ujenzi wa miundombinu ya urushaji wa matangazo katika mfumo wa
dijitali unaendana na ratiba ya uhamiaji katika mfumo wa matangazo kutoka mfumo
wa analojia kwenda dijitali, taarifa za mara kwa mara zimekuwa zikiletwa na
wajenzi wa miundombinu hiyo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na
kujadiliwa na Kamati mbalimbali zinazohusiana na masuala ya uhamaji katika
mfumo wa utangazaji wa dijitali. Taarifa hizo zimekuwa zikionyesha kuwa ujenzi
wa miundombinu unaendelea vizuri na kwamba ratiba ya uzimaji wa mitambo ya
analojia nchini itakwenda kama ilivyokubalika na wadau wa utangazaji.
Kufuatia
uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kuelimisha umma kuhusu mabadiliko ya mfumo wa
utangazaji kutoka katika mfumo wa analojia na kwenda katika mfumo wa dijitali
uliofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali, kwa
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, iliandaa Mkakati Maalum wa Mawasiliano ambao ulilenga katika kuhamasisha
wananchi kuhusu uhamaji katika mfumo wa utangazaji wa dijitali. Njia mbalimbali
zimetumika katika kuelimisha umma kuhusu mabadiliko ya mfumo wa utangazaji
ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali, kutoa
vipeperushi na matangazo katika magazeti, redio na televisheni, kufanya
majadiliano katika televisheni na redio ambayo yalihusisha pia maswali kutoka
kwa wadau mbalimbali, kuweka taarifa katika tovuti kuhusu masuala mbalimbali ya
uhamaji katika mfumo wa utangazaji.
Taarifa
zilizopo zinaonyesha kuwa uhamasishaji na elimu kwa umma imetolewa kwa kiasi
kikubwa na wananchi wamehamasika sana katika kuingia katika mfumo wa utangazaji
wa dijitali kutoka ule wa analojia. Hii ni kutokana na wananchi wengi
kujitokeza kununua ving’amuzi (visimbuzi) kwa
wingi katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ambayo matangazo katika
mfumo wa analojia yalitarajiwa kuzimwa. Aidha, hapakuwa na mapendekezo yoyote kutoka kwa wajenzi wa miundombinu ya
urushaji wa matangazo ya dijitali kuwa watashindwa kujenga miundombinu hiyo
kwa wakati ifikapo tarehe 31 Desemba 2012, siku ambayo ilikuwa imekubalika
kuzima mitambo ya utangazaji ya mfumo wa analojia na kuanza kutumia mfumo wa
dijitali. Tarehe 31 Desemba 2012, Serikali ilianza kuzima matangazo hayo kwa
awamu ili kubaini na kushughulikia changamoto mbalimbali ambazo zingeweza
kujitokeza katika mabadiliko hayo.
Uzimaji
wa mitambo ya utangazaji wa analojia kwenda katika mfumo wa utangazaji wa
dijitali ilianza kutekelezwa tarehe 31 Desemba 2012 kwa kuzima mitambo 14 ya
televisheni inayotumia utangazaji wa mfumo wa analojia katika jiji la Dar es
Salaam ambapo wananchi wengi walinunua ving’amuzi
ili waweze kujiunga na mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali. Kadhalika, uzimaji
wa mitambo ya analojia kwenye miji ya Dodoma na Tanga ulifanyika tarehe 31
Januari 2013. Uzimaji wa mitambo ya analojia kwa jiji la Mwanza ulifanyika
tarehe 28 Februari 2013. Uzimaji wa mitambo kwa miji ya Arusha na Moshi
umefanywa tarehe 31 Machi 2013. Kwa ujumla wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa
wingi kujiunga na mfumo huu mpya wa utangazaji na hakuna matatizo
yaliyojitokeza zaidi ya changamoto kadhaa ambazo zimeendelea kupatiwa ufumbuzi.
Ikumbukwe
kuwa uzimaji wa urushaji wa matangazo katika mfumo wa analojia na kuanza
kutumika kwa mfumo wa dijitali umefanywa mahali ambapo kuna mawimbi (signal) ya
televisheni ya dijitali tu. Pale ambapo hakuna mawimbi ya televisheni ya
dijitali, matangazo ya televisheni yameendelea kurushwa katika mfumo wa
analojia hadi wakati ambapo mawimbi ya televisheni ya dijitali yatakapofikia
mahali hapo. Hivyo, kwa mfano katika Jiji la Mwanza ambapo urushaji wa
matangazo katika mfumo wa dijitali ulisitishwa tarehe 28 Februari 2013, maeneo
yaliyoguswa na usitishaji wa matangazo hayo ni Mwanza City, Sengerema, Ukerewe
na Kisesa. Sehemu nyingine zote za Mkoa wa Mwanza bado zinaendelea kupokea
matangazo ya televisheni katika mfumo uliokuwepo hapo awali. Vivyo hivyo,
uzimaji wa matangazo katika Jiji la Tanga umegusa maeneo ya Jiji la Tanga,
Muheza, Mkanyageni, Nguvu Mali, Mabokweni na Mkinga. Maeneo mengine kama vile
Lushoto, Korogwe, Handeni yanaendelea kupokea matangazo katika mfumo uliokuwa
unatumika hapo awali. Hivyo, katika maeneo ambayo hakuna uzimaji wa mitambo ya
analojia umefanywa, wananchi wanaendelea kupata matangazo ya televisheni kwa
kutumia mfumo uliokuwepo hapo awali.
Serikali
inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa katika maeneo ambayo tayari kuna matanagzo
ya televisheni katika mfumo wa dijitali, watumiaji wa televisheni wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanapata matangazo ya televisheni zote zenye leseni za kitaifa
bila gharama yoyote ile ya ziada mbali na gharama ya kununua king’amuzi (kisimbuzi) ambacho
kinawezesha kuona matangazo katika mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali.
Stesheni hizo ni TBC1, ITV, Star TV, Channel 10, na East African TV. Endapo
matangazo ya televisheni ya vituo hivyo hayapatikani, wananchi wawasiliane mara
moja na wato huduma za ving’amuzi ili kuwasaidia
kupatia ufumbuzi.
Serikali
inatumia fursa hii, kuwashukuru na kuwapongeza wananchi kwa kuitikia vyema wito
wa kuhamia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali katika maeneo yote
yaliyohusika na uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa analojia. Aidha, Serikali
inavishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari ambavyo vimekuwa mstari wa mbele
katika kuelimisha umma kuhusu mabadiliko haya ya mfumo wa utangazaji. Serikali
itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kwa kutumia njia mbalimbali, ili
Tanzania iwe imekamilisha uhamiaji katika mfumo mpya wa utangazaji kabla ya
tarehe 17 Juni 2015.
Hata hivyo, katika siku
za hivi karibuni, Serikali imeshuhudia kauli mbalimbali
zinazotolewa na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari na hasa wa utangazaji
kupitia vyombo vya habari wanavyovimiliki, wakiilaumu na kuishutumu Serikali
kuhusu uamuzi halali wa Serikali wa kuhamia katika mfumo wa dijitali. Kauli
hizo zilizotolewa kwa nguvu kupitia mikutano ya waandishi wa habari na pia
kuhusisha mijadala katika baadhi ya redio na televisheni zina nia ya kufifisha
mchakato wa uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda mfumo wa
dijitali.
Kauli
hizi sio za kweli, zinapotosha ukweli na hali halisi na pia zinalenga kuchochea
wananchi kutokubaliana na maamuzi haya ya Serikali na pia kutounga mkono juhudi
za Serikali ilizokwishafanya katika kutekeleza azma ya uhamaji kutoka
utangazaji wa mfumo wa analojia kwenda dijitali. Kauli hizo si tu
zimewachanganya wananchi wanaoendelea kuhamia katika mfumo mpya utangazaji wa
dijitali, bali pia zimetia hofu vyombo vya fedha ambavyo vimekuwa vikitoa
mikopo kwa wajenzi wa miundombinu ya urushaji wa matangazo katika mfumo wa
dijitali. Madhara ya kauli hizo ni kuwapotosha wananchi kuhusu suala zima la
uhamiaji katika mfumo wa utangazaji wa dijitali na pia kukwamisha juhudi za
Serikali kuhakikisha zoezi la kuhamia dijitali linafanikiwa kabla ya kufikia
ukomo wa matangazo ya analojia tarehe 17 Juni 2015.
Serikali
inapenda kuwafahamisha wananchi kwa mara nyingine tena, Serikali ilifikia
maamuzi ya kuhamia dijitali kwa kuzingatia maslahi ya taifa wananchi msikubali
kupotoshwa kwa ajili ya maslahi binafsi. Upotoshaji huu unaweza kusababisha
wananchi kukosa taarifa muhimu ikiwa ni pamoja na kupata taarifa mbalimbali za
maendeleo au matukio ya ndani na nje ya nchi; kufuatilia mijadala bungeni na
pia kufuatilia mchakato wa kuandaa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, upotoshaji unaofanywa unaweza kusababisha hasara kubwa kwa wananchi
ambao wataendelea kununua televisheni zinazotumia mfumo wa analojia. Vile vile,
upotoshaji huo utachelewesha wananchi kutumia huduma nyingine nyingi
zinazoendana na teknolojia ya utangazaji ya dijitali ikiwa ni pamoja na huduma
za Intaneti, huduma za kifedha, ununuzi wa vitu kwa njia ya mtandao na kupata
chaneli nyingine za ziada.
Baadhi
ya wamiliki hao wa vyombo vya habari wanatambua wazi kuwa walikuwa na fursa kwa
zaidi ya miaka 7 kuwasilisha maoni au malalamiko yao kwa vyombo husika ili kama
kuna changamoto katika uhamiaji huo ziweze kufanyiwa kazi, badala ya kutumia
muda mwingi wa matangazo katika vyombo vyao vya habari kupotosha umma kuhusu
dhana nzima na mchakato wa uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia
kwenda dijitali. Kwa kuwa upotoshaji huu unaongozwa na wamiliki wa vyombo vya
habari ambavyo kwa namna moja au nyingine vinahusika na ujenzi wa miundombinu
ya urushaji wa matangazo katika mfumo wa dijitali, Serikali iko tayari
kushirikiana na wadau hao katika kutatua changamoto zinazowakabili ili
kuhakikisha kuwa utekelezaji wa uhamiaji katika mfumo wa utangazaji unaendelea
kama ilivyopangwa badala ya kutumia muda mwingi kuupotosha umma.
Ikumbukwe
kuwa mabadiliko haya hayaepukiki, hivyo basi wadau wote kwa pamoja hawana budi
kushirikiana katika mchakato mzima kama ilivyokubalika kupitia vikao mbalimbali
vilivyofanyika toka mwaka 2005 vikishirikisha wadau wote wa Sekta ya
Utangazaji, wakiwemo wamiliki wote wa vyombo vya habari vya utangazaji wa
televisheni nchini. Serikali imejiridhisha kuwa mchakato wote wa kuelekea mfumo
wa utangazaji ulifanywa kwa umakini mkubwa na kwa muda wa kutosha, elimu
imetolewa na inaendelea kutolewa. Aidha, ni dhahiri kuwa watoa huduma za miundombinu
ya dijitali waliopewa leseni tangu 2010 wameendelea na wajibu wa kuweka mitambo
ya dijitali sehemu mbalimbali nchini na zoezi linaendelea vizuri.
Serikali
haitavumilia kikundi au mtu yeyote atakayeonekana kupotosha au kufifisha
mchakato wa kuhamia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali. Aidha, Serikali
inaiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuendelea na utaratibu, ratiba ya
zoezi zima la uzimaji wa mitambo ya analojia kama ilivyotolewa na Serikali.
Vile vile, Serikali inaiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kupitia Kamati ya
Maudhui kuchunguza endapo kauli zilizotolewa na baadhi ya wamiliki wa vyombo
vya habari kwa kutumia muda mrefu kuelezea kauli zao katika vyombo vyao vya
habari kama hawakukiuka sheria na kanuni za Utangazaji kwa nia ya kupotosha
umma kwa kusudio la kudhoofisha maamuzi haya ya Serikali.
Pamoja
na tathmini ya awali ambayo Serikali, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
imefanya na kuonyesha kuwa mchakato wa uhamaji unaendelea vizuri, Serikali
itafanya tathmini ya kina baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya uzimaji wa
mitambo ya kurushia matangazo ya analojia kwenye miji 7 ambayo kwa sasa inapata
matangazo kupitia mfumo wa utangazaji wa dijitali. Tathmini hiyo itaendana na
kufanya mkutano wa wadau wote wa utangazaji nchini ili kuweza kupata maoni yao
kabla ya kuanza awamu ya pili ya uzimaji kwenye miji 14 ambayo itapata huduma
za matangazo ya dijitali hivi karibuni.
Serikali
inaomba wananchi kupuuza upotoshaji unafanywa kuhusu ukweli wa mabadiliko ya
mfumo wa utangazaji wa kutoka analojia kwenda dijitali. Aidha, tunaomba vyombo
vya habari kuendelea kutoa ushirikiano na kuendelea kuunga mkono juhudi hizi
muhimu kwa kuelimisha umma kuhusu ukweli katika mchakato wa uhamiaji katika
mfumo wa utangazji wa dijitali. Serikali itaendelea kupokea maoni kutoka kwa
wadau ili kuhakikisha kuwa uhamiaji unakamilika mapema kabla ya ukomo wa
matangazo ya analojia tarehe 17 Juni 2015.
Imetolewa na:
Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.)
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
DAR ES
SALAAM
2 Aprili 2013
Harrah's Casino - Mapyro
Harrah's Cherokee Casino Resort features 속초 출장마사지 over 2,300 slot machines and 83 table games. 안동 출장샵 Cherokee, 속초 출장마사지 NC, USA 777 Casino 광명 출장안마 Drive, Murphy, NC 서울특별 출장마사지 28906-1000.