Mstahiki
Meya wa Ilala, Mhe. Jerry Slaa, akimkabidhi cheti cha Ushindi wa Jumla, Kaimu
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala
*******
Mamlaka ya Mawasiliano Nchini, TCRA, imeshinda Tuzo
ya Tasisi Bora ya Mawasiliano ya Kifedha nchini, baada ya kuibuka na ushindi wa
jumla kwenye maonyesho ya Seta ya Fedha nchini, yaliyomalika jana, kwenye
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Ushindi huo wa TCRA, umepatikana kufuatia makampuni
, Asasi na Tasisi za kifedha nchini, zilizoshiriki katika maonysho hayo,
kupimwa jinsi huduma zake zinavyosaidia ukuaji wa sekta ya fedha nchini, ambapo
TCRA imeibuka na ushindi huo kufuatia kutoa vibali na number maalum kwa
makampuni ya simu na taasisi za kifedha nchini kutumia number number hizo kwa
huduma za kifedha, ziitwazo SIM Banking, kulikopekea Watanzania wengi zaidi
kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya rahisi zaidi .
Ushindi wa pili umetwaliwa na kampuni ya simu za
mkoni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa ikielezewa hii ndio huduma ya
pesa iliyosambaa nchini kote na kutumiwa na mamilioni ya Watanzania kama
mkombozi wao katika huduma za kifedha.
Kwa upande wa mabenki, Benki ya CRDB ndio imeshinda
kama benki kiongozi katika maonyesho hayo kwa kuwa ndio benki pekee hapa nchini,
iliyoshiriki maonyesho hayo kwa kishindo kikubwa kwa kuwakilishwa na benki
yenyewe ya CRDB PLC na kampuni yake tanzu ya CRDB Microfinance LTD iliyoelezwa
kuwa ndio benki pekee iliuyowafikia wajasiliamali wadodo wadogo wa vijini
kuliko benki nyingine yoyote.
Akielezea, ushindi huo una maan a gani kwa TCRA,
Mkuu wa Huduma za Elimu kwa Umma wa CRDB, Issack Mruma, amesema ushindi huo ni
motisha kwa TCRA kuzidi kutoa huduma bora zaidi za mawasiliano nchini na kueleza
umekuja wakati muafaka na sambamba na Tanzania kuchaguliwa kuingia kwenye Bodi
ya Shirika la Posta Ulimwenguni UPU katika mkutano unaendeleo huko Doha, Falme
za Kiarabu.
Akipokea Tuzo hiyo, Kaimu Meneja Mawasiliano wa
TCRA, Semu Mwakiyanjala, amesema ushindi huo, unawapa faraja angalau kwa TCRA
kutambulika nyumbani kuwa ni mabingwa wa maendeleo ya sekta ya mawasiliano sio
nchini tuu bali barani Afrika.
“Unajua Nabii huwa hathaminiwi nyumbani, sisi TCRA
tunaongoza sana katika huduma bora za mawasiliano barani Afrika na duniani kwa
ujumla, nchi nyingi zinakuja kujifunza kwetu, hati kazi ya upangaji wa maswafa
dunuani, TCRA inategemewa sana kuwapangia masafa nchi nyingine kule kwenye ITU”
alisema Mwakiyanjala.
Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa TCRA na Mstahiki Meya wa
Ilala, Mhe. Jerry Slaa, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho hayo
baada ya maonyesho ya siku nne ya taasisi za fedha nchini yaliyoandaliwa na
kampuni ya Neubrand.