Mabadiliko
katika mfumo wa utangazaji kutoka mfumo wa analojia kwenda katika mfumo wa dijitali
ni utaratibu ambao unaendelea ulimwenguni kote. Mabadiliko haya yanatokana na
makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya
masuala ya mawasiliano yaani International
Telecommucations Union yaliyofanyika mwaka 2005 huko Geneva, Uswisi.
Makubaliano ya nchi wanachama ni kuzima kabisa matangazo katika mfumo wa
analojia na kutumia mfumo wa utangazaji wa dijitali ifikapo tarehe 17 Juni
2015.
Ili
kuhakikisha mabadiliko haya yanafanyika kwa ufanisi, tija na pia kutoa muda wa
kutosha wa kutekeleza mabadiliko haya, mwaka 2005 Serikali ilianza mchakato wa
uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali ambao ulihusisha
wadau wote, wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari na vituo vya utangazaji wa
televisheni, hatua kwa hatua, hadi kuridhia ratiba nzima ya uzimaji wa mitambo
ya analojia. Kwa kifupi mchakato wa uhamaji ulipitia hatua zifuatazo: